Wiki ya Afya 2025: Tulipotoka, Tulipo na Tunapoelekea
Wizara ya Afya yenye dhamana ya kusimamia huduma za afya nchini imeandaa maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza, lengo likiwa ni kuufahamisha umma wa Watanzania maboresho yaliyofanyika katika sekta ya Afya nchini. Maadhimisho haya yanatarajiwa kuanza tarehe 03 Aprili, 2025 hadi tarehe 8 Aprili, 2025 jijini Dodoma.